Thursday, November 27, 2014

UFAHAMU UGONJWA WA ZINAA WA TRICHOMONIASIS AMBAO HUWAATHIRI SANA WANAWAKE



 Ugonjwa wa Trichomoniasis ni mojawapo ya ugonjwa ulio katika kundi la magonjwa ya zinaa zaidi ya 25 yanayofahamika kwa watu wengi.Ugonjwa huu huwaathiri sana wanawake kuliko wanaume.Ugonjwa huu wa Trichomoniasis unasababishwa na vimelea vya jamii ya protozoa vinavyojulikana kama Trichomonas Vaginalis ambao huathiri mrija wa kupitishia mkojo(urethra)na tupu ya mwanamke.Trichomoniasis pia hujulikana kwa majina mengine kama Trichomonas Vaginitis au Trich.
Ugonjwa huu huathiri watu milioni 170 kwa mwaka duniani kote .Nchini Marekani pekee ambayo imeendelea katika fani ya tiba watu milioni 8 huambukizwa ugonjwa huu.Ugonjwa huu huonekana sana kwa wanawake kuliko wanaume kutokana na wanaume kutoonyesha dalili zozote wakati wa maambukizi au kutokana na majimaji ya kwenye tezi dume kuwa na madini ya Zinc ambayo huathiri vimelea hivi vya Trichomonas Vaginalis vinavyosababisha ugonjwa huo.

MAAMBUKIZI;
Trichomoniasis huambukizwa kwa njia ya kujamiiana bila kutumia kinga na mtu aliyeathiriwa na ugonjwa huo.Wanawake wengi wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa huu ,ili kuufahamu ugonjwa huu vyema kwanza tufafamu nini kinachotokea wakati wa maambukizi(PATHOFIZIOLOJIA)ya ugonjwa huu.
-Umbile la vimelea vya Trichomonas Vaginalis ni sawa na chembechembe moja ya damu nyeupe  kwa upana ingawa wakati mwingine ukubwa unaweza kutofautiana kulingana na mazingira.
-Kuwepo kwa umbile kama mikono kwa nje ya kwenye kimelea hicho inayojulikana kama FLAGELLUM ,husaidia vimelea hivi kuingia kwenye tishu za mrija wa kupitishia mkojo na tupu ya mwanamke na hivyo kuharibu seli aina ya EPITHELIUM na kusababisha vidonda katika tishu hizo hali ambayo husababisha watu walioathirika na ugonjwa huu kuwa kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa VVU na magonjwa mengine ya zinaa.
Trichomoniasis huanza kuonekana kuanzia siku ya 4-28 baada ya mtu kupata maambukizi.Kwa wanawake Trichomoniasis huathiri shingo ya kizazi (cervix),mrija wa mkojo,tupu ya mwanamke,kibofu cha mkojo na tezi zinazojulikana kama BARTHOLIN Glands na Skene Glands.
-Kwa wanaume vimelea hivi hupatikana katika sehemu za siri,sehemu ya nje ya mrija wa kupitishia mkojo(Anterior Urethra),kwenye tezi dume,kwenye mirija ya kuhifadhi na kutoa mbegu za kiume(EPIDIDYMIS) na hata kwenye mbegu zenyewe.

DALILI KWA WANAWAKE;
1.Uchafu unaotoka kwenye tupu ya mwanamke ambao huwa na rangi mchanganyiko ya njano na kijani au rangi kama kijivu na huwa mzito sana.
2.Maumivu wakati wa tendo la ndoa
3.Kutoka harufu kwenye tupu ya mwanamke
4.Maumivu wakati wa kujisaidia haja ndogo
5.Shingo ya kizazi kuwa nyekundu hali ambayo hugundulika wakati daktari anamfanyia mgonjwa uchunguzi
6.Kuwashwa sehemu za siri(sio wanawake wote)
7.Maumivu chini ya kitovu kwa baadhi ya wanawake
Ingawa wanawake ndio huonyesha dalili na viashiria vya ugonjwa huu mara nyingine wanaweza kuwa na vimelea hivi hata kwa muda wa miaka kadhaa hata kama vipimo vya uchunguzi havitaonyesha kama wameathirika na vimelea vya ugonjwa huu.

DALILI KWA WANAUME;
Baadhi ya wanaume huwa hawaonyeshi dalili zozote .Baadhi ya dalili zinazoonekana ni;
1.Kuwashwa ndani ya uume
2.Kutokwa na uchafu au majimaji kwenye uume
3.Kuwashwa au kuhisi kichomi baada ya kujisaidia haja ndogo au baada ya kutoa mbegu za kiume
Baada ya mtu kuhisi dalili hizo anashauriwa kwenda hospitali au katika vituo vya afya ili kufanyiwa uchunguzi na vipimo.
VIPIMO;
Trichomoniasis hugundulika kwa kutumia vipimo
1.Kipimo cha darubini ambapo daktari humfanyia mgonjwa uchunguzi kwa kuingiza kifaa maalum katika tupu ya mwanamke na kuchukua kipimo kwa kutumia pamba maalum.Hatua hii hufanywa kitaalam bila kusababisha maumivu kwa mgonjwa na kisha kupelekwa maabara ili kuangalia kama kuna vimelea vya Trichomonas Vaginalis.Kwa kufanya uchunguzi huu daktari anaweza pia kuangalia kama kuta za ndani za tupu ya mwanamke au shingo ya kizazi (cervix) zimeathirika kwa kuwa na vidonda ambavyo ni vyekundu.
2.Kwa mwanaume daktari huchukua kipimo cha uchafu unaotoka sehemu za siri au hupangusa sehemu hizo za siri za mwanaume kwa wale ambao hawatoi uchafu au majimaji yoyote kwa kutumia pamba na kupeleka maabara kufanyia uchunguzi.Pia kipimo kilichochukuliwa na daktari kinaweza kuoteshwa kwenye maabara(culture) na kuangalia kama kuna uoto wa vimelea vya Trichomonas Vaginalis baada ya siku tatu.
3.Kuangalia kiwango cha tindikali(PH)-daktari anaweza kuangalia kiwango cha tindikali kwenye tupu ya mwanamke kwa kutumia karatasi maalum ya kkipimo hiki ijulikanayo kama PH paper,ambapo kiwango kama ameathirika itakuwa PH zaidi ya 5.Kwa kawaida PH ya tupu ya mwanamke inakuwa ni ya tindikali(acidic) kuanzia PH 3.8-4.5 .Magonjwa yanayobadilisha PH ni pamoja na;Trichomoniasis na Bacteria Vaginosis.Mabadiliko hayo humfanya mwanamke kuwa kwenye hatari ya maambukizi tofauti.
4.Kipimo cha damu -hufanywa ili kuchunguza Prostate Specific Antigen(PSA).PSA ni aina ya protin inayozalishwa na seli za tezi dume.Uzalishaji wake huongezeka wakati seli za tezi dume zinapoongezeka kuelekea kuwa kansa inayojulikana kitaalam kama BPH au wakati tezi dume inapopata maambukizi(PROSTITIS),na katika saratani ya tezi dume.Kipimo hiki hufanywa kwa wanaume wanaopata ugonjwa wa Trichomoniasis mara kwa mara au wale wenye umri kuanzia miaka 60 na kuendelea na ambao wamepata ugonjwa huu wanapaswa kufanyiwa kipimo hiki angalau mara 1 kwa mwaka.
5.Pap smear -hiki ni kipimo kingine ambapo chembechembe au seli za shingo ya kizazi huchukuliwa na kuchunguzwa kwa kutumia darubini.Kipimo hiki pia hutumiwa katika uchunguzi wa wanawake kujua kama wamepata saratani ya shingo ya kizazi au la.Wanawake wenye zaidi ya miaka 18 au wale wenye upungufu wa kinga ya mwili wanashauriwa kufanya kipimo hiki angalau mara 1 kwa mwaka ili kujua afya zao.
6.Kipimo cha kuangalia maambukizi ya VVU-walioathirika na Trichomoniasis wanapaswa kufanyiwa kipimo cha kuangalia kama wameambukizwa ugonjwa wa HIV.
7.Kipimo cha mkojo na damu-hufanywa kuangalia wingi wa damu,chembechembe tofauti za damu na chembechembe bapa(Platelets)

MATIBABU;
Tiba ya trichomoniasis ni kutumia dawa aina ya Metronidazole au Flagyl.Dawa hii haitumiki kwa wanawake wenye ujauzito chini ya miezi 3 au wanaonyonyesha hivyo basi kabla ya kutumia dawa hii ni vyema ukamuona daktari.Kwa wale walioathirika na ugonjwa huu wa zinaa wanashauriwa kupata tiba pamoja na wenzi wao .Madhara mengine ya dawa ya Metronidazole mbali na madhara kwa wamama wajawazito na wanaonyonyesha ni pamoja na;
1.Mzio(mcharuko wa mwili)yaani allergic reaction
2.Kichefuchefu
3.Kukauka midomo
4.Kuharisha
5.Kuhisi ladha kama ya chuma mdomoni
6.Kushuka kiwango cha chembechembe nyeupe za damu(leukopenia)ambazo hutoa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali na hivyo upungufu wake hufanya mtu awe  katika hatari ya kupata maambukizi tofauti tofauti.Mcharuko wa dawa hii mara nyingi hutokea iwapo masharti ya dawa hayakufatwa vyema au mtu anapokunywa dozi ya dawa zaidi ya alivyoelekezwa na daktari.Ni muhimu kufahamu kuwa unapohisi hali kama hizo katika matibabu yoyote inakupasa kuacha kutumia dawa zinazokudhuru na kumuona daktari haraka.
Katika kituo chetu cha LMTM HERBAL CENTRE tunazo dawa za mimea zisizi na kemikali zozote na isiyo na madhara kwa wajawazito na wanyonyeshao yenye uwezo wa kutibu siyo Trichomoniasis pekee bali magonjwa yote sugu ya zinaa kama kaswende,kisonono,klamidia,UTI n.k.Dawa hiyo inajulikana kwa jina la LMTM-N7/SUZ.Kwa wale waliofika katika kituo chetu ni mashahidi wa uwezo wa dawa hii kutibu magonjwa yote ya zinaa.
NB;LMTM HERBAL CENTRE ndicho kituo pekee ndani ya Tanzania,Afrika mashariki kati na kusini mwa Afrika chenye uwezo wa kutibu magonjwa ya zinaa sugu na uzazi.

MADHARA YA TRICHOMONIASIS;
1.Ugonjwa huu ni miongoni ya magonjwa ya zinaa ambayo huongeza hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa mengine kama HIV kama tulivyokwisha sema huko nyuma.
2.ugonjwa huu husababisha mwanamke kujifungua mtoto mwenye uzito mdogo
3.Huwaongezea wanawake hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi
4.Kuongeza hatari kwa wanaume kupata saratani ya tezi dume.


Maintained by an  ICT consultant and Director of Studies:  IFF YOU NEED HELP PLZ CALLA US VIA 0782 474941 0767 4749411 OR VIST www.kcckibaha.blogspot.com kcckimisha@gmail.com

No comments:

Post a Comment