CHUKUA VITAWI VYA UKUBWA WA KAWAIDA VYENYE IDADI YA 11
KISHA CHEMSHA KWENYE SUFURIA KUBWA CHEMSHA VITAWI HIVYO KWA MUDA WA DAKIKA 45 kisha mimina kwenye chombo cha kuogea oga maji hayo yakiwa bado ya motomoto {vuguvugu} fanya zoezi hili kutwa mara mbili kwa muda wa siku tano 5
Maajabu Tiba ya Muarobaini
Ndugu msomaji, Unaujua muarobaini...?
Wengi wetu watasema wanaujua lakini hawajui maana ya kuitwa muarobaini
mti huo kwa kuwa mti huu ulipandwa nchini kwa amri ya kila nyumba kuwa
na miti hii japo miwili huku wenye maeneo ya biashara wakihimizwa
kuupanda mti huu kwa masharti kuwa asiyepanda basi atanyang’anywa
leseni!
Si maneno ya mtu mwingine bali Kanali Yusuph Makamba ambaye aliwahi kuwa
mkuu wa mkoa huu wa Dar Es Salaam enzi hizo za mwanajeshi huyu
alipopata wazo la kuleta mbegu hii toka nchini India na kuupandikiza
kijeshi-jeshi maana anatujua fika watanzania kwa ubishi usio na maana
hata kwa maslahi yetu wenyewe.
Leo hii hasa vipindi hivi vya jua kali utakuta watu wote wapo chini ya
muarobaini wakipata oksijeni nyiiingi tu toka kwenye mti huo jeuri bila
kumbukumbu kuwa ulipandwa kwa viboko! Lakini, Angalau dozi ya malaria
sasa inagusa mitaa ya shilingi elfu kumi na zaidi huku watanzania bado
wanashindwa kutegua kitendawili cha mwanajeshi huyu mstaafu. Yeye
amemaliza kazi:
Alikoutoa huo mti nchini India, unaitwa village Pharmacy na mlipomuuliza
huu ni mti gani aliwajibu kuwa huu ni muarobaini na alijua mtalishika
hili jina hadi mtakaposhindwa kumudu gharama za mahospitalini basi kila
mtu atajua mwarobaini ni nini kwa kuwa utatibu maradhi yote
yatakayotusumbua watanzania na kutunusuru na gharama hizi kubwa za
madawa ya kemikali mahospitalini.
Nasikitika kuwa inawezekana siku tutakapolijua hili pengine mtaalamu
huyu toka jeshi la Tanzania anaweza akawa kaburini na tukabaki na
historia yetu ya kutangaza wema wa mtu baada ya kifo chake…
Muarobaini ukikamuliwa juisi yake umethibitishwa na vyuo vikuu vya tiba
duniani kuwa una uwezo wa kukinga maambukizi ya HIV nap engine kutibu
kabisa ugonjwa wa UKIMWI ambao husababishwa na virusi vya HIV.
Muarobaini una uwezo mkubwa wa kuzuia aleji na kutibu pia aleji za aina
tofauti kama juisi yake itapakwa mwilini na hata kama utainywa pia.
Muarobaini huko Marekani na India umeonyesha uwezo mkubwa wa kuzuia
nyani dume kutoa mbegu za uzazi kwa majike na kugundulika kuwa juisi ya
muarobaini inamfaa mwanaume anayetaka kupanga uzazi bila kwenda
hospitali kwa vipimo, ushauri na kufanyiwa upasuaji mdogo kukinga
uzalishaji wa mimba (Vasectomy)
Muarobaini pia ni kiboko kwa wanawake wasio na mpango wa kushika mimba
vilevile. Muarobaini kama utakamuliwa juisi yake na kupakwa kwenye via
vya uzazi vya mwanamke , basi juisi hiyo itamsaidia mwanamke kutopata
mimba zisizotarajiwa.
Muarobaini una uwezo mkubwa wa kupambana na kansa na hata kinga ya mwili
pia. Tindikali ziitwazo Polysaccharides na limonoids zilizomo katika
magamba, majani na mizizi huboresha kinga ya mwili haraka mno ili
kupambana na maradhi kama kansa na mengineyo bila uharibifu wa mwili
kama zilivyo dawa kemikali za mahospitalini.
Muarobaini hutibu kisukari kwa haraka sana. Majani matatu tu ya
muarobaini ni dozi tosha kwa mgonjwa wa kisukari na akizidisha zaidi ya
matatu basi anaweza kurudi hospitali na kuwaomba tena waganga waitafute
sukari kwenye damu yake kwa tochi! Maana muarobaini utaikomba sukari
yote kwenye damu hivyo usijiongezee dozi kijinga.
Muarobaini hushambulia wadudu wote wanaoshambulia ngozi ya binadamu kwa
usahihi kabisa. Muarobaini hutibu mapunye, mba, ukurutu, upele na
magonjwa kadhaa ya ngozi bila madhara yoyote.
Muarobaini hutibu magonjwa ya moyo. Huifanya damu kuwa nyepesi itembee
kwa mwendo sahihi na kuyafanya mapigo ya moyo kuwa tulivu kwa wenye
maradhi ya moyo.
Mafua.
Ujerumani ambako ni nchi ya baridi kwa kipindi kirefu cha majira ya
mwaka watu hufa kwa mafua tu! Tafiti walizofanya zinasema juisi ya
muarobaini hukata mafua haraka zaidi ya dawa yoyote ya hospitalini huku
ikikuhakikishia usalama bila madhara.
Muarobaini unaua fangasi. Inawezekana una fangasi miguuni, kwenye
maungio ya siri kama mapajani, kwapani, sehemu za siri n.k. tumia juisi
ya muarobaini ujipake sehemu zilizoathirika kupambana na fangasi hao
bila madhara.
Muarobaini pia ni dawa ya kufukuza wadudu bila madhara ya kemikali.
Jaribu kulala chini ya muarobaini lakini angalia pawe na majani yake
hapo chini halafu utaona hakuna usumbufu wa mbu wala nzi maana
mwarobaini hufukuza wadudu aina kadhaa akiwemo mbu!
Wakala wa kulinda mazingira Marekani imeupitisha muarobaini kama kinga
bora ya kuhifadhia mazao dhidi ya wadudu waharibifu huku ikidaiwa kwamba
muarobaini hauna sumu mara 200 zaidi ya madawa ya kemikali na mazao
yanakuwa salama kwa matumizi ya binadamu,ndege na wanyama kwa ujumla.
Muarobaini pia hutibu malaria. Mchanganyiko maalum wa majani ya
muarobaini uitwao kwa kitaalam “irodin A” ni sumu ya kuzuia na kutibu
malaria. Majaribio mengi yamefanyika hata hapa nchini na muarobaini
umeonekana una nguvu ya kupambana na malaria hata hapa nchini Tanzania
japo si mti wenye asili yetu.
Nilipoingia katika tiba asili, wataalamu wengi waliniambia kama nataka
mafanikio ya haraka basi nianze na kutibu wagonjwa kwa muarobaini. Naapa
kwa watanzania wote kuwa nilifanikiwa sana maana hakuna aliyerudi
akasema hakupona ugonjwa wowote hivyo nina imani siku mwarobaini
ukitumika kama India basi utaitwa National Pharmacy….
Na nina wasiwasi kuwa kama wadau wa afya wakichelewa kuwajulisha wenye
nchi taarifa hii muhimu tena kwa vituo basi watakapogundua hili,
matabibu wengi watakosa ajira maana hakuna atakayeenda tena hospitali:
akatafute nini?
Maana hata urafiki kati ya matabibu na wenye nchi utapungua kwa kuwa
watagundua kuwa walifichwa habari hizi ili wawe mitaji ya wadau wa afya
ambao ni sisi! Binafsi nimeanzisha kozi ya kutengeneza vidonge vya
muarobaini inayogharimu shilingi elfu sitini tu kwa wenye familia zenye
msimamo na tiba asili ili kesho niweze kujitetea kuwa nilijitahidi kwa
uwezo wangu kusambaza taarifa hizi kwa vitendo.
No comments:
Post a Comment