Miski ni mfalme wa aina zote za mafuta mazuri na ni matukufu zaidi.Ni
mafuta ambayo hupigiwa mfano mzuri kwa kufadhilishwa kuliko mafuta
mengine.
SIFA ZA MISKI;
-Miski hali yake ina joto na inauyabisi katika daraja la pili.
-Ina harufu na ladha yake ni tofauti na mafuta mazuri mengine.Ukitaka
kutofautisha miski feki na halisi,ni kwamba katika tiba za kimwili miski
feki haiwezi kutibu maradhi maduka mengi yanauza miski feki ambazo sio
zile zilizokusudiwa kutuka katika tiba.Ikiwa unahaja ya tiba hakikisha
umeata miski asilia.
TIBA ZA MISKI;
1.Huchangamsha na kusafisha mishipa ya fahamu na ubongo.
2.Huongeza hisia,ashiki na ladha za tendo la ndoa kwasababu huzidisha matamanio na joto mwilini
3.Huwasaidia wanawake wasiokuwa na ashki(hisia) na ladha wakati wa tendo
la ndoa.Tunayo pia dawa ya ziada ya kuongeza nguvu,hisia na hamu
yatendo la ndoa kwa wanawake dawa hii ulizia katika kituo chetu cha lmtm
herbal centre.
4.Huwasaidia wanaume wanaowahi kumaliza tendo la ndoa kabla ya mke.Namna
ya kutumia wasiliana na wataalam wetu waliopo katika kituo chetu
kilichopo ilaa cha lmtm herbal centre.Kwa ziada ya haya tunazo dawa
zingine za kuongeza nguvu za kiume ambazo ni za kunywa na za kuchua kwa
kuimarisha na kuipa nguvu mishipa ya dhakal.Dawa hii pia ni mujarab kwa
kuchelewesha kuwahi kutoa manii haraka
5.Husaidia wanawake waliomaliza siku zao za hedhi kuondoa harufu mbaya.Pia hupunguza umajimaji na harufu mbaya itokayo ukeni
6.Hukazanisha utupu wa mwanamke na kufanya sehemu hiyo kuwa ndogo
kcc tiba herbs research
Friday, November 28, 2014
IMARISHA UWEZO WA KUFANYA TENDO LA NDOA KWA KULA MATUNDA NA MBOGAMBOGA
Ili mtu awe na afya bora na hatimaye aweze kumudu tendo la ndoa ni lazima mwili wake upate virutubisho kama vile;
a.wanga
b.mafuta
c.protini
d.vitamin na madini kwa kiwango sahihi kutoka katika chakula
Moja ya sababu ya mtu kupoteza hamu na nguvu ya kufanya tendo la ndoa ni msongo mzito wa mawazo.Msongo wa mawazo unaufanya mwili kushindwa kuzalisha kiwango tosha la vichocheo ya kufanya tendo la ndoa.Kwahiyo hamu na nguvu ya kufanya tendo la ndoa inapungua.Sababu nyingine inayosababisha mtu kukosa hamu na nguvu ya tendo la ndoa ni vyakula.
Ili mwanaume aweze kuwa na hamu na nguvu ya kufanya tendo la ndoa lazma tezi dume lake liwe na afya bora.Madini ya zinki ambayo hupatikana kwa urahisi katika maharage,vitunguu,matango,karoti,spinachi,kabichi na matunda mbalimbali husaidia kufanya tezi dume kuwa imara.
Baadhi ya vitamini kama;
1.vitamini A inayopatikana kwa wingi katika spinachi,karoti,matikiti na maembe.Inaweza kubadili lehemu kuwa kichocheo madhubuti katika kufanya tendo la ndoa.
2.vitamini B inayopatikana kwa wingi katika viazi,ndizi na maboga husaidia kutengeneza vichocheo katika tendo la ndoa
3.vitamini E inayopatikana kwa wingi katika vyakula vya asili kama vile pumba za ngano,majani machanga ya mtama,ufuta na matunda ya aina mbalimbali kwa kiasi kikubwa inaimarisha maisha ya mu katika kufanya tendo la ndoa kwa muda mrefu.Upungufu wa vitamini E mwilini unaweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume mwilini.
Ulaji wa ndizi unasaidia kupunguza msongo wa mawazo kwa sababu ya kuwa na madini ya potassium kwa wingi ambayo husababisha mwili kuongezeka kwa wingi vichocheo vya tendo la ndoa.Kwa mwanaume kazi moja ya tezi za dume ni kutoa majimaji yaliyochanganyika na mbegu za kiume wakati wa kufanyika tendo la ndoa.
Baadhi ya watu hutumia dawa au hormonies ili kuongeza nguvu ya kufanya tendo la ndoa.Matumizi ya aina zozote za dawa yana changamoto zake,ikiwemo madhara ya kiafya na kiuchumi hivyo watu wanashauriwa kujenga tabia ya ulaji bora na kufanya mazoezi ili kuweza kukabili tatizo hilo.Ulaji wa kudumu wa matunda na mbogamboga au juisi za asili unaimarisha afya na kumpa mtu nguvu na hamu ya kufanya tendo la ndoa. Hata hivyo ieleweke kuwa kuna baadhi ya watu kama vile wasiozalisha vichocheo,tiba yao sio chakula pekee bali ni lazma waende hospitalini kufanyiwa vipimo na kup[atiwa tiba sahihi kulingana na tatizo walilonalo.
Tahadhari:matumizi holela ya madawa yanaweza kuleta madhara katika figo au kudhoofisha kabisa nguvu ya kufanya tendo la ndoa.
Maintained by an ICT consultant and Director of Studies: IFF YOU NEED HELP PLZ CALLA US VIA 0782 474941 0767 4749411 OR VIST www.kcckibaha.blogspot.com kcckimisha@gmail.com
Mawe katika figo na athari zake kiafya
Ni tatizo ambalo linasumbua wengi lakini ambalo halifahamiki vizuri
Tumesikia habari mbalimbali zinazohusu tatizo hili na dhana mbalimbali ambazo zimekuwa zikijengwa.
Hata hivyo, baadhi ya watu hukumbwa na tatizo la kuwa na vijiwe katika figo na mfumo wa mkojo kwa jumla.
Mawe haya hutokana ama madini, chumvi au tindikali
mbalimbali zinazotolewa mwilini. Nchini Tanzania, baadhi ya wagonjwa
hushtuka wakielezwa wana tatizo hili wakidhani labda wamerogwa, ila
jambo la msingi watambue hili ni tatizo la kiafya.
Aina za mawe katika figo
Aina za vijiwe katika figo ni pamoja na vijiwe vya
calcium oxalate, vijiwe vya tindikali ya uriki (uric acid), vijiwe vya
struvite (magnesium, ammonium na phosphate)
Sababu za vijiwe katika figo
Kwa kiasi kikubwa, vijiwe husababishwa na
kukosekana kwa usawa wa maji, madini na tindikali mwilini, ambayo
kitaalamu huitwa electrolyte imbalance.
Kuna magonjwa kadhaa ambayo husababisha kwa kiasi
kikubwa kutokea kwa hali hii kama ugonjwa wa utindikali kwenye mirija ya
figo, matatizo kwenye tezi za shingo, kukojoa chumvi chumvi za oxalate
kupita kiasi na hali ya nyama za figo kuwa tepetepe.
Nani yupo hatarini?
Tatizo hili huwapata zaidi watu walio na historia
ya familia zao kuwa na vijiwe kwenye figo, walio na umri kuanzia miaka
40 au zaidi, ingawa tatizo hili linaweza kutokea katika umri wowote.
Pia, linaweza kuwapata wanaume zaidi kuliko
wanawake, wana upungufu wa maji mwilini, kwa lugha rahisi wale
wasiopenda kunywa maji katika kiwango kinachoshauriwa.
Huwatokea wale wanaopendelea kula zaidi vyakula vyenye kiasi
kikubwa cha protini, chumvi au/na sukari, walio na unene kupita kiasi,
walio na magonjwa ya utumbo mkubwa au waliowahi kufanyiwa upasuaji wa
tumbo.
Dalili zake
Kujihisi kichefuchefu, kutapika, kukojoa mkojo
uliochanganyika na damu. Wakati mwingine uwepo wa usaha katika mkojo
hasa iwapo kuna maambukizi ya bakteria, Maumivu wakati wa kukojoa.
Mkojo kutoka kwa kiwango kidogo, mkojo hushindwa
kupita katika mirija ya ureter na kusababisha figo kushindwa kutoa
uchafu mwilini na kusababisha mlundikano wa uchafu kwenye damu hali
inayojulikana kama postrenal azotemia, kushindwa kupita kwa mkojo
husababisha pia kutanuka kwa sehemu tofauti za figo na iwapo kutakuwa
na maambukizi katika mkojo, mgonjwa anaweza kuhisi kuwa na homa
Vipimo na uchunguzi
Vipimo vinavyoweza kugundua tatizo hili na madhara
yake ni pamoja na x-ray inayoonyesha mfumo mzima wa figo, mirija ya
figo kwenda katika kibofu-ureta pamoja na kibofu cha mkojo.
Kipimo kingine huitwa intravenous pyelogram (IVP),
vipimo vya CT-scan au MRI, ultrasound ya tumbo, kipimo cha mkojo na
kuotesha, kipimo cha damu (FBP)
Matibabu yake
Matibabu ya vijiwe katika figo hutegemea na ukubwa
wa vijiwe husika. Iwapo vijiwe vina ukubwa mdogo na dalili alizo nazo
mgonjwa ni chache na hazimzuii kuendelea na kazi zake za kila siku,
mgonjwa anashauriwa kunywa maji mengi kiasi cha lita 2 mpaka 3 kwa siku.
Hii husaidia kuviondoa vijiwe kutoka katika figo
au njia ya mkojo na kutumia dawa za maumivu ili kupunguza maumivu iwapo
yatatokea
Iwapo vijiwe ni vikubwa na dalili ni nyingi na
zinamfanya mgonjwa ashindwe kuendelea na kazi zake za kila siku, mgonjwa
anaweza kutibiwa kwa kutumia tiba zifuatazo:
Mawimbi mshtuko kutoka nje ya mwili ili
kuvunjavunja vijiwe na kisha vijiwe hivyo hutolewa nje kupitia kwenye
mkojo, upasuaji na kisha kuvitoa vijiwe, kifaa maalumu kiitwacho
ureteroscope, wakati mwingine upasuaji wa kuondoa tezi za parathyroid
hufanyika.
Jinsi ya kuzuia tatizo hili
Mambo unayoweza kufanya kuzuia tatizo la vijiwe
kwenye figo ni pamoja na kunywa maji mengi kwa siku na kuhakikisha
unakojoa angalau lita 2.5 za mkojo kila siku.
Punguza utumiaji wa vyakula vyenye oxalate kama
viazi vitamu, spinachi, soya, chai na chocolate, kula vyakula vyenye
chumvi kidogo na punguza protini hasa itokanayo na nyama, hivyo tumia
itakonayo na jamii ya kunde na maharage.
Potassium citrate husaidia kuongeza pH hivyo
kuzuia wingi wa tindikali katika mwili. Kwa walio na tatizo la
uzalishaji uliopitiliza wa tindikali ya uriki, wanaweza kushauriwa
kutumia dawa aina ya Allopurinol.
Maintained by an ICT consultant and Director of Studies: IFF YOU NEED HELP PLZ CALLA US VIA 0782 474941 0767 4749411 OR VIST www.kcckibaha.blogspot.com kcckimisha@gmail.com
Maintained by an ICT consultant and Director of Studies: IFF YOU NEED HELP PLZ CALLA US VIA 0782 474941 0767 4749411 OR VIST www.kcckibaha.blogspot.com kcckimisha@gmail.com
ZIJUE DALILI,TIBA NA UCHUNGUZI WA TATIZO LA MAWE KWENYE FIGO
TATIZO LA MAWE KWENYE FIGO(KIDNEY STONES)
-Figo ni kiungo muhimu katika mwili wa binadamu,hufanya kazi ya kuchuja damu huku ikiondoa sumu zote za mwili,figo hufanya kazi ya kurekebisha kiasi cha maji mwilini(electrolyte level).
kabla damu haijapita katika figo,huwa imebeba maji na takataka nyingi sana(urea),lakini inapopita katika figo huchujwa na vitu muhimu hurudishwa katika mzunguko wa damu lakini,masalia mengine ambayo hayafai tena katika mwili ikiwa ni pamoja na kiwango cha maji kilichozidi hupitishwa kwenye mirija miwili(ureters)kuelekea kwenye kibofu(urinary bladder) na kishas kutolewa nje ya mwili kupitia njia ya mkojo(urethra)
Mkusanyiko wa kemikali hizi(chemical crystals),wakati mwingine hugandamana na kutengeneza chembechembe ya vitu kama mchanga,kadri siku zinavyozidi kuendelea ndivyo vinavyozidi kukua hadi wengine hufikia hatua ya kuziba njia ya mkojo katika figo yenyewe(neprone) au kwenye mirija ya kupeleka mkojo kutoka kwenye figo kwenda kwenye kibofu(ureteter),hapo ndipo mtu anaanza kupata shida ya kukojoa na kusikia maumivu makali.
DALILI ZA UWEPO WA MAWE KWENYE FIGO;
Mtu mwenye mawe kwenye figo huonyesha dalili zifuatazo;
a.Maumivu ya mgongo na kiuno
b.Mkojo kutoka ukiwa na rangi ya damu
c.Kutokwa na jasho wakati wa usiku
d.Kupatwa na homa kali kwa wakati flani ikiambatana na kutetemeka mwili
e.Kuhisi kichefuchefu na kutapika
f.Mkojo kuwa na harufu kali
g.Maumivu makali sehemu za mbavu
h.Miguu kujaa maji/kuvimba.
i.Maumivu ya tumbo chini ya kitovu upande wa kushoto au kulia kutegemea ni figo ya upande gani iliyoathirika.
j.Maumivu makali unapogusa upande wa figo iliyoathirika.
KISABABISHI CHA MAWE KATIKA FIGO(KIDNEY STONES);
1.Matumizi ya baadhi ya dawa husababisha mtu kupata mawe katika figo pindi anapozitumia kila mara.Dawa hizo ni kama vile za kutibu kansa na HIV,antibiotic kama ciprofloxacin,cefrtriaxone na madawa yenye sulphur kama metacalphin nk.
2.Utumiaji wa vyakula vyenye kuongeza vitamin A na D,ambavyo huongeza kwa kiasi kikubwa madini joto mwilini
3.Kuishi kwenye mazingira ya joto sana bila kupata maji ya kutosha husababisha kiasi cha chemical kuongezeka katika figo na kusababisha zigandamane na kutengeneza mawe ndani ya figo.
4.Maambukizi ya magonjwa ya figo kama renal tubula acidocis ctc,huongeza hatari ya kupata tatizo hilo.
5.Kurithi kutoka kwa wazazi (wanakuwa na homoni ziitwazo antiduretic hormone)zisizoweza kufanya kazi ya kuchuja damu kikamilifu na mwishowe hutengeneza mawe katika figo.
6.Utumiaji wa vyakula vyenye protin zinazotokana na wanyama na chumvi nyingi(huongeza hatari ya kupata tatizo hili)
7.Unene kupita kiasi
JINSI YA KUGUNDUA TATIZO;
1.Mgonjwa kufanyiwa X-Ray au scan ili kujua kama ana mawe katika figo.
2.Vipimo vya damu(blood test)
3.Vipimo vya mkojo(urenarlulisis)
TIBA YA TATIZO;
-Ikiwa mgonjwa baada ya uchunguzi atagundulika kuwa na tatizo hili hupewa mojawapo ya tiba zifuatazo:
1.Extracorporeal shock wave lithotripys(eswl)-Hii ni mionzi inayoelekezwa katika figo ili kuyeyusha mawe (chemical au sumu zilizogandamana)ambazo huvunjwavunjwa na hii mionzi kisha mgonjwa hukojoa vipandevipande.
2.Percutaneous nephrolithotomy(PCNL)-Hiki ni kifaa chenye mwanga na kamera ambacho huingizwa kwenye kokwa za figo (nephrone)ambayo huvunjavunja mawe katika figo.
3.Ureteroscopy-Kifaa hiki huingizwa kwenye mirija ya kupitishia mkojo(urether)kutoka kwenye figo kwenda kwenye kibofu ili kuondoa mawe yaliyokwama kwenye mirija na kuzuia mkojo kutoka.
4.Stone removal-Hapa mgonjwa hufanyiwa operesheni ya kuondoa mawe moja kwa moja.
- Kama tulivyoona tiba hizi zina madhara na ni ghali.Hivyo basi kabla hujaenda katika tiba hizi zenye madhara makubwa ni muhimu kutumia tiba mbadala na tiba asili ili kuepuka madhara mengine.
Katika kituo chetu cha LMTM HERBAL CENTRE tunayo dawa asili zenye uwezo mkubwa wa kutibu tatizo hili la mawe kwenye figo bila madhara yoyote.Aina hizi za dawa hufanya kazi za kuyeyusha kemikali na mafuta yaliyogandamana katika figo na kuzibua mirija iliyojiziba ili kuruhusu mtiririko wa mkojo kuwa kama unavyotakiwa.
Baadhi ya madawa tuliyonayo ni;
a.LMTM-F5/AFH2
b.LMTM/S32/J
Dawa hizi mbali na kutibu matatizo ya mawe katika figo zinauwezo wa;
1. kutibu saratani ya kizazi,kusafisha mirija ya uzazi na kutoa maji katika mirija hiyo
2.Uvimbe wowote ndani ya mwili
3.Kurekebisha hedhi iliyovurugika kwa akina mama(hasa waliowahi kutumia dawa za uzazi wa mpango)
4.Saratani ya ini na kibofu cha mkojo
5.Kusafisha mfumo mzima wa njia ya mkojo
6.Huwasaidia akina mama wenye kasoro mbalimbali katika via vya uzazi,waotafuta uzazi kupata watoto
Maintained by an ICT consultant and Director of Studies: IFF YOU NEED HELP PLZ CALLA US VIA 0782 474941 0767 4749411 OR VIST www.kcckibaha.blogspot.com kcckimisha@gmail.com
Thursday, November 27, 2014
UNATAKA KUPUNGUZA UNENE ?SOMA HII HAPA
Hapa nakuletea ratiba ya kupunguza unene/uzito kwa muda wa siku saba kwa kutumia lishe maalum;
(1)Siku ya kwanza asubuhi kula matunda(lakini katika matunda hayo usile ndizi).Mchana chemsha kabichi,weka chumvi kidogo na nyanya na upate supu kisha kula mchanganyiko huo.Jioni kula tikiti maji na mboga mboga au kabichi uliyotengeneza mchana.
(2) Siku ya pili kula mboga za majani asubuhi (usile mboga za majani zenye wanga kama karoti).Mchana kula kabichi iliyochemshwa ,tengeneza na kachumbari.katika kabichi weka chumvi,pilipili na mafuta ya olive.Jioni unaweza kula mlo kama wa mchana lakini unaweza kukaanga mboga nyingine za majani.
(3)Siku ya tatu kula mboga za majani na matunda ,unaweza kuongeza kiazi kitamu kimoja .
(4)Siku ya nne kula ndizi moja na unywe na maziwa ya mtindi wakati wa asubuhi ,Mchana kula kabichi kama ulivyoitengeneza kwenye siku ya kwanza,usiku rudia mlo wa mchana.
(5)Siku ya tano kula nyanya nn pamoja na samaki au kipande cha kuku asubuhi.Mchana unaweza kula samaki wa kuchemsha kiasi ambaye amechanganywa na nyanya.Wakati wa jioni unaweza kula chakula kama cha mchana.
(6)Siku ya sita unaweza kula chakula cha protin na mboga za majani.Anza siku kwa kula kachumbari asubuhi.Mchana kula tambi kiasi na kipande kidogo cha samaki.Usiku tengeneza supu ya kabichi.
(7)Siku ya saba anza kwa matunda na juisi,Mchana kula mboga za majani na usiku kula supu ya kabichi na kiazi kimoja.
NB:Unatakiwa kunywa maji angalau glasi nne kila siku.Dayati hii ni kwa siku saba tu.
Maintained by an ICT consultant and Director of Studies: IFF YOU NEED HELP PLZ CALLA US VIA 0782 474941 0767 4749411 OR VIST www.kcckibaha.blogspot.com kcckimisha@gmail.com
(1)Siku ya kwanza asubuhi kula matunda(lakini katika matunda hayo usile ndizi).Mchana chemsha kabichi,weka chumvi kidogo na nyanya na upate supu kisha kula mchanganyiko huo.Jioni kula tikiti maji na mboga mboga au kabichi uliyotengeneza mchana.
(2) Siku ya pili kula mboga za majani asubuhi (usile mboga za majani zenye wanga kama karoti).Mchana kula kabichi iliyochemshwa ,tengeneza na kachumbari.katika kabichi weka chumvi,pilipili na mafuta ya olive.Jioni unaweza kula mlo kama wa mchana lakini unaweza kukaanga mboga nyingine za majani.
(3)Siku ya tatu kula mboga za majani na matunda ,unaweza kuongeza kiazi kitamu kimoja .
(4)Siku ya nne kula ndizi moja na unywe na maziwa ya mtindi wakati wa asubuhi ,Mchana kula kabichi kama ulivyoitengeneza kwenye siku ya kwanza,usiku rudia mlo wa mchana.
(5)Siku ya tano kula nyanya nn pamoja na samaki au kipande cha kuku asubuhi.Mchana unaweza kula samaki wa kuchemsha kiasi ambaye amechanganywa na nyanya.Wakati wa jioni unaweza kula chakula kama cha mchana.
(6)Siku ya sita unaweza kula chakula cha protin na mboga za majani.Anza siku kwa kula kachumbari asubuhi.Mchana kula tambi kiasi na kipande kidogo cha samaki.Usiku tengeneza supu ya kabichi.
(7)Siku ya saba anza kwa matunda na juisi,Mchana kula mboga za majani na usiku kula supu ya kabichi na kiazi kimoja.
NB:Unatakiwa kunywa maji angalau glasi nne kila siku.Dayati hii ni kwa siku saba tu.
Maintained by an ICT consultant and Director of Studies: IFF YOU NEED HELP PLZ CALLA US VIA 0782 474941 0767 4749411 OR VIST www.kcckibaha.blogspot.com kcckimisha@gmail.com
UFAHAMU UGONJWA WA ZINAA WA TRICHOMONIASIS AMBAO HUWAATHIRI SANA WANAWAKE
Ugonjwa wa Trichomoniasis ni mojawapo ya ugonjwa ulio katika kundi la magonjwa ya zinaa zaidi ya 25 yanayofahamika kwa watu wengi.Ugonjwa huu huwaathiri sana wanawake kuliko wanaume.Ugonjwa huu wa Trichomoniasis unasababishwa na vimelea vya jamii ya protozoa vinavyojulikana kama Trichomonas Vaginalis ambao huathiri mrija wa kupitishia mkojo(urethra)na tupu ya mwanamke.Trichomoniasis pia hujulikana kwa majina mengine kama Trichomonas Vaginitis au Trich.
Ugonjwa huu huathiri watu milioni 170 kwa mwaka duniani kote .Nchini Marekani pekee ambayo imeendelea katika fani ya tiba watu milioni 8 huambukizwa ugonjwa huu.Ugonjwa huu huonekana sana kwa wanawake kuliko wanaume kutokana na wanaume kutoonyesha dalili zozote wakati wa maambukizi au kutokana na majimaji ya kwenye tezi dume kuwa na madini ya Zinc ambayo huathiri vimelea hivi vya Trichomonas Vaginalis vinavyosababisha ugonjwa huo.
MAAMBUKIZI;
Trichomoniasis huambukizwa kwa njia ya kujamiiana bila kutumia kinga na mtu aliyeathiriwa na ugonjwa huo.Wanawake wengi wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa huu ,ili kuufahamu ugonjwa huu vyema kwanza tufafamu nini kinachotokea wakati wa maambukizi(PATHOFIZIOLOJIA)ya ugonjwa huu.
-Umbile la vimelea vya Trichomonas Vaginalis ni sawa na chembechembe moja ya damu nyeupe kwa upana ingawa wakati mwingine ukubwa unaweza kutofautiana kulingana na mazingira.
-Kuwepo kwa umbile kama mikono kwa nje ya kwenye kimelea hicho inayojulikana kama FLAGELLUM ,husaidia vimelea hivi kuingia kwenye tishu za mrija wa kupitishia mkojo na tupu ya mwanamke na hivyo kuharibu seli aina ya EPITHELIUM na kusababisha vidonda katika tishu hizo hali ambayo husababisha watu walioathirika na ugonjwa huu kuwa kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa VVU na magonjwa mengine ya zinaa.
Trichomoniasis huanza kuonekana kuanzia siku ya 4-28 baada ya mtu kupata maambukizi.Kwa wanawake Trichomoniasis huathiri shingo ya kizazi (cervix),mrija wa mkojo,tupu ya mwanamke,kibofu cha mkojo na tezi zinazojulikana kama BARTHOLIN Glands na Skene Glands.
-Kwa wanaume vimelea hivi hupatikana katika sehemu za siri,sehemu ya nje ya mrija wa kupitishia mkojo(Anterior Urethra),kwenye tezi dume,kwenye mirija ya kuhifadhi na kutoa mbegu za kiume(EPIDIDYMIS) na hata kwenye mbegu zenyewe.
DALILI KWA WANAWAKE;
1.Uchafu unaotoka kwenye tupu ya mwanamke ambao huwa na rangi mchanganyiko ya njano na kijani au rangi kama kijivu na huwa mzito sana.
2.Maumivu wakati wa tendo la ndoa
3.Kutoka harufu kwenye tupu ya mwanamke
4.Maumivu wakati wa kujisaidia haja ndogo
5.Shingo ya kizazi kuwa nyekundu hali ambayo hugundulika wakati daktari anamfanyia mgonjwa uchunguzi
6.Kuwashwa sehemu za siri(sio wanawake wote)
7.Maumivu chini ya kitovu kwa baadhi ya wanawake
Ingawa wanawake ndio huonyesha dalili na viashiria vya ugonjwa huu mara nyingine wanaweza kuwa na vimelea hivi hata kwa muda wa miaka kadhaa hata kama vipimo vya uchunguzi havitaonyesha kama wameathirika na vimelea vya ugonjwa huu.
DALILI KWA WANAUME;
Baadhi ya wanaume huwa hawaonyeshi dalili zozote .Baadhi ya dalili zinazoonekana ni;
1.Kuwashwa ndani ya uume
2.Kutokwa na uchafu au majimaji kwenye uume
3.Kuwashwa au kuhisi kichomi baada ya kujisaidia haja ndogo au baada ya kutoa mbegu za kiume
Baada ya mtu kuhisi dalili hizo anashauriwa kwenda hospitali au katika vituo vya afya ili kufanyiwa uchunguzi na vipimo.
VIPIMO;
Trichomoniasis hugundulika kwa kutumia vipimo
1.Kipimo cha darubini ambapo daktari humfanyia mgonjwa uchunguzi kwa kuingiza kifaa maalum katika tupu ya mwanamke na kuchukua kipimo kwa kutumia pamba maalum.Hatua hii hufanywa kitaalam bila kusababisha maumivu kwa mgonjwa na kisha kupelekwa maabara ili kuangalia kama kuna vimelea vya Trichomonas Vaginalis.Kwa kufanya uchunguzi huu daktari anaweza pia kuangalia kama kuta za ndani za tupu ya mwanamke au shingo ya kizazi (cervix) zimeathirika kwa kuwa na vidonda ambavyo ni vyekundu.
2.Kwa mwanaume daktari huchukua kipimo cha uchafu unaotoka sehemu za siri au hupangusa sehemu hizo za siri za mwanaume kwa wale ambao hawatoi uchafu au majimaji yoyote kwa kutumia pamba na kupeleka maabara kufanyia uchunguzi.Pia kipimo kilichochukuliwa na daktari kinaweza kuoteshwa kwenye maabara(culture) na kuangalia kama kuna uoto wa vimelea vya Trichomonas Vaginalis baada ya siku tatu.
3.Kuangalia kiwango cha tindikali(PH)-daktari anaweza kuangalia kiwango cha tindikali kwenye tupu ya mwanamke kwa kutumia karatasi maalum ya kkipimo hiki ijulikanayo kama PH paper,ambapo kiwango kama ameathirika itakuwa PH zaidi ya 5.Kwa kawaida PH ya tupu ya mwanamke inakuwa ni ya tindikali(acidic) kuanzia PH 3.8-4.5 .Magonjwa yanayobadilisha PH ni pamoja na;Trichomoniasis na Bacteria Vaginosis.Mabadiliko hayo humfanya mwanamke kuwa kwenye hatari ya maambukizi tofauti.
4.Kipimo cha damu -hufanywa ili kuchunguza Prostate Specific Antigen(PSA).PSA ni aina ya protin inayozalishwa na seli za tezi dume.Uzalishaji wake huongezeka wakati seli za tezi dume zinapoongezeka kuelekea kuwa kansa inayojulikana kitaalam kama BPH au wakati tezi dume inapopata maambukizi(PROSTITIS),na katika saratani ya tezi dume.Kipimo hiki hufanywa kwa wanaume wanaopata ugonjwa wa Trichomoniasis mara kwa mara au wale wenye umri kuanzia miaka 60 na kuendelea na ambao wamepata ugonjwa huu wanapaswa kufanyiwa kipimo hiki angalau mara 1 kwa mwaka.
5.Pap smear -hiki ni kipimo kingine ambapo chembechembe au seli za shingo ya kizazi huchukuliwa na kuchunguzwa kwa kutumia darubini.Kipimo hiki pia hutumiwa katika uchunguzi wa wanawake kujua kama wamepata saratani ya shingo ya kizazi au la.Wanawake wenye zaidi ya miaka 18 au wale wenye upungufu wa kinga ya mwili wanashauriwa kufanya kipimo hiki angalau mara 1 kwa mwaka ili kujua afya zao.
6.Kipimo cha kuangalia maambukizi ya VVU-walioathirika na Trichomoniasis wanapaswa kufanyiwa kipimo cha kuangalia kama wameambukizwa ugonjwa wa HIV.
7.Kipimo cha mkojo na damu-hufanywa kuangalia wingi wa damu,chembechembe tofauti za damu na chembechembe bapa(Platelets)
MATIBABU;
Tiba ya trichomoniasis ni kutumia dawa aina ya Metronidazole au Flagyl.Dawa hii haitumiki kwa wanawake wenye ujauzito chini ya miezi 3 au wanaonyonyesha hivyo basi kabla ya kutumia dawa hii ni vyema ukamuona daktari.Kwa wale walioathirika na ugonjwa huu wa zinaa wanashauriwa kupata tiba pamoja na wenzi wao .Madhara mengine ya dawa ya Metronidazole mbali na madhara kwa wamama wajawazito na wanaonyonyesha ni pamoja na;
1.Mzio(mcharuko wa mwili)yaani allergic reaction
2.Kichefuchefu
3.Kukauka midomo
4.Kuharisha
5.Kuhisi ladha kama ya chuma mdomoni
6.Kushuka kiwango cha chembechembe nyeupe za damu(leukopenia)ambazo hutoa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali na hivyo upungufu wake hufanya mtu awe katika hatari ya kupata maambukizi tofauti tofauti.Mcharuko wa dawa hii mara nyingi hutokea iwapo masharti ya dawa hayakufatwa vyema au mtu anapokunywa dozi ya dawa zaidi ya alivyoelekezwa na daktari.Ni muhimu kufahamu kuwa unapohisi hali kama hizo katika matibabu yoyote inakupasa kuacha kutumia dawa zinazokudhuru na kumuona daktari haraka.
Katika kituo chetu cha LMTM HERBAL CENTRE tunazo dawa za mimea zisizi na kemikali zozote na isiyo na madhara kwa wajawazito na wanyonyeshao yenye uwezo wa kutibu siyo Trichomoniasis pekee bali magonjwa yote sugu ya zinaa kama kaswende,kisonono,klamidia,UTI n.k.Dawa hiyo inajulikana kwa jina la LMTM-N7/SUZ.Kwa wale waliofika katika kituo chetu ni mashahidi wa uwezo wa dawa hii kutibu magonjwa yote ya zinaa.
NB;LMTM HERBAL CENTRE ndicho kituo pekee ndani ya Tanzania,Afrika mashariki kati na kusini mwa Afrika chenye uwezo wa kutibu magonjwa ya zinaa sugu na uzazi.
MADHARA YA TRICHOMONIASIS;
1.Ugonjwa huu ni miongoni ya magonjwa ya zinaa ambayo huongeza hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa mengine kama HIV kama tulivyokwisha sema huko nyuma.
2.ugonjwa huu husababisha mwanamke kujifungua mtoto mwenye uzito mdogo
3.Huwaongezea wanawake hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi
4.Kuongeza hatari kwa wanaume kupata saratani ya tezi dume.
Maintained by an ICT consultant and Director of Studies: IFF YOU NEED HELP PLZ CALLA US VIA 0782 474941 0767 4749411 OR VIST www.kcckibaha.blogspot.com kcckimisha@gmail.com
JE WAJUA KUWA VYOMBO VYA PLASTIKI NI MOJAWAPO YA VYANZO VYA SARATANI ?SOMA HAPA
- Ili kupunguza uwezekano huo unashauriwa
(1)Usinywe chai kwa kutumia vikombe vya plastiki
(2)Usile chochote chenye moto kilichofungwa ndani ya mfuko wa plastiki kama chips nk.
(3)Usipashe chakula ndani ya microwave kwa kutumia chombo cha plastiki
(4)Epuka kuchoma mabaki ya plastiki sehemu wanakoishi watu kwani ukivuta moshi huo ni hatari na pia inaweza kusababisha saratani ya mapafu nk
Maintained by an ICT consultant and Director of Studies: IFF YOU NEED HELP PLZ CALLA US VIA 0782 474941 0767 4749411 OR VIST www.kcckibaha.blogspot.com kcckimisha@gmail.com
Subscribe to:
Posts (Atom)